Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, sambamba na maadhimisho ya miaka 1,500 tangu kuzaliwa Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.), Wiki ya Umoja, pamoja na kufanyika kwa sehemu ya kielimu ya Mkutano wa 40 wa Umoja wa Kiislamu mjini Qum, “Mkusanyiko wa Juzuu 12 ukiwa na Mada za Utafiti wa Elimu na Maarifa ya Kimuhammadi (s.a.w.w.)” umezinduliwa mbele ya Ayatullah Arafi, Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu nchini Iran, na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Baraza la Kimataifa la Kuleta Ukaribu wa Madhehebu ya Kiislamu.
Kubadilisha Maarifa ya Kimuhammadi Kuwa Nadharia Zinazotumika
Katika mkusanyiko huu wenye thamani, maswali na masuala 60,000 za utafiti katika mada na nyanja mbalimbali za kielimu, yanayozingatia changamoto na maswali ya zama hizi kuhusu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.), yameainishwa, kuwasilishwa na kupangwa katika makundi. Aidha, juhudi zimefanywa kubaini na kuchunguza mapengo pamoja na mielekeo mipya ya kielimu katika uwanja wa tafiti kuhusu Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), na kuchunguza namna hadithi na maarifa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) yanavyoweza kubadilishwa kuwa nadharia zinazotumika na kutekelezeka katika vitendo.
Zawadi ya Hawza za Kielimu kwa Jamii
“Mkusanyiko wa Juzuu 12 wa Mada za Utafiti wa Elimu na Maarifa ya Kimuhammadi (s.a.w.w.)”, ambao unahesabiwa kuwa kazi ya kipekee katika ulimwengu wa Kiislamu, umetolewa na Hawza ya Qum pamoja na wafuasi wa Madhehebu ya Amirul-Mu’minina (a.s.), kwa baraka ya kuwepo kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), kuwa zawadi kwa jamii ya kibinadamu, watafiti wa dini na watafiti wanaojishughulisha na masomo ya Mtume.
Hatua hii ni ya kwanza, na katika hatua zinazofuata, masuala haya yatawekewa vipaumbele, yatafafanuliwa na kufuatiliwa, kisha yatabadilishwa kuwa matokeo ya kielimu katika mfumo wa makala, vitabu, vikao vya kielimu, majukwaa ya fikra huru na uundaji wa nadharia.
Mtazamo Mpya wa Kistaarabu na Kielimu Kumhusu Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w.)
Mkusanyiko huu adhimu wa kielimu, ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa Hawza ya Qum, Naibu Uongozi wa Masuala ya Kimataifa, Naibu Uongozi wa Utafiti, pamoja na Sekretarieti ya Kusaidia Tafiti Zinazohitajika kwenye Hawza na Mfumo, unaweza kuwa msingi wa mtazamo mpya wa kistaarabu na kisayansi kumhusu Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w.), na kuweka mazingira ya kuimarisha ukaribu pamoja na mshikamano wa kielimu katika ulimwengu wa Kiislamu.







Maoni yako